2 Chronicles 3:1-6

Sulemani Ajenga Hekalu

(1 Wafalme 6:1-38; 7:15-22)

1 aNdipo Sulemani akaanza kujenga Hekalu la Bwana katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, pale ambapo Bwana alikuwa amemtokea Daudi baba yake. Ilikuwa katika kiwanja cha kupuria cha Arauna,
Pia anaitwa Ornani kwa Kiebrania.
Myebusi, mahali palipotolewa na Daudi.
2 cAlianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa utawala wake.

3 dMsingi aliouweka Sulemani kwa ajili ya kulijenga Hekalu la Mungu ulikuwa urefu wa dhiraa sitini
Dhiraa 60 ni sawa na mita 27.
na upana dhiraa ishirini.
Dhiraa 20 ni sawa na mita 9.
4 gUkumbi wa mbele wa Hekalu ulikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, yaani, kuanzia upande mmoja hadi upande mwingine wa upana wa nyumba hiyo na kimo chake dhiraa thelathini.
Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5.

Akaufunika ndani kwa dhahabu safi.
5 iAkaufunika ukumbi mkuu kwa mbao za miberoshi na kufunikwa kwa dhahabu safi na kuupamba kwa miti ya mitende na kuifanyizia kwa minyororo. 6Alilipamba Hekalu kwa vito vya thamani. Hiyo dhahabu aliyotumia ilikuwa dhahabu ya Parvaimu.
Copyright information for SwhKC